Chris Mauki Awashauri Vijana Kutokuogopa Kuvunja Mahusiano Au Uchumba.

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Mtaalamu Wa Maswala Ya Saikolojia Ya Jamii Na Mwalimu Katika Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam Leo Amewashauri Vijana Kutokuogopa Kuvunja Mahusiano Au Uchumba Kwa Sababu Ya Kukaa Muda Mrefu Katika Mahusiano.

Pia Amewatia Moyo Na Kuwaonyesha Vijana Kuwa Bado Inawezekana Kuanzisha Mahusiano Mapya Na Yenye Furaha Na Kuchomoka Kwenye Mahusiano Yenye Maumivu Na Machozi Kila Mara.

Ameandika;

“Maranyingine kwenye mahusiano unaweza kuhofia kuvunja mahusiano au uchumba na mtu kwasababu umekaa naye muda mrefu na unahofia kuanzisha mahusiano mapya na mtu mpya, moyoni unajiambia ile methali ya zimwi likujualo halikuli likakwisha, kwamba hatakama huyu uliyenaye anamapungufu basi ngoja nivumilie labda huyo mpya anaweza kunipa shida zaidi. Ngoja nikwambie, hakunaga formula kwenye mahusiano, unaweza kuhofia kuachana naye kwasababu ya muda mliokaa naye kumbe penzi lilishavunda halafu mkishaoana mbeleni ndio unakuja kugundua kuwa zimwi likujualo kumbe linaweza kukutafuna likakumaliza kabisa. Inawezekana kabisa kuanzisha mahusiano yenye furaha na kuchomoka kwenye mahusiano yenye maumivu na machozi kila mara. Fanya maamuzi bora kabla haujaingia kwenye ndoa maana huko madhara ya kuvunjika ni makubwa zaidi #ChrisMauki”.

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter , Instagram Na Youtube “johnpazia”ili kupata habari Kutoka Kila Kona Ya Mitaa Mbalimbali Duniani Live On Live Masaa 24 Kila Siku.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*