Pastor Nick Shaboka Aeleza Aina Mbili Za Wanawake. Asema Kuna Ngazi Na Kaburi.

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 22
    Shares

Mchungaji Nick Shaboka Wa Kanisa La New Day Church, Sinza A Ameelezea Aina Mbili Za Wanawake Ambao Wapo Katika Jamii.

Katika Ujumbe Wake Ameandika;

“KUNA AINA MBILI ZA WANAWAKE.

NGAZI NA KABURI.

Aina ya kwanza ni NGAZI (Ladder/Staircase/Elevator/Escalator). Ngazi ni kifaa kilichotengenezwa mahususi kusaidia kupandia au kushukia kutoka eneo la juu sana kusikofikika kirahisi kwa kuzingatia usalama wa mtumiaji. NGAZI ipo kurahisa upandaji ambao ungeng’ang’ana na kuchukua muda mrefu kufika, NGAZI inakufikasha haraka. NGAZI za kielekroniki huwezesha watu kwenda hata ghorofa ya 120 kwa dakika chache.
MWANAMKE wa aina ya NGAZI anapoingia kwenye maisha ya Mwanaume, mara huyu Mwanaume huanza kubadilika kwa kuwa bora kila siku. Kama anakipawa au kipaji kitaanza kung’aa na kuchukua muelekeo chanya. Atabadilika hata mavazi na makazi na heshima yake itaongezeka. Sio lazima sana mwanamke wa aina ya NGAZI kuwa na pesa, ila anakuwa na ushauri unaomfanya Mwanaume wake kufanikiwa kila akiufuata. Na hata kama hana ushauri bado uwepo wake kwenye maisha ya Mwanaume wake husababisha amani ya moyo na utulivu wa kichwa unaomfanya Mwanaume kupambana kujikwamua na kufikia ndoto zake na kubadilisha maisha. Ukibahatika kupata mwanamke wa namna hii, kila siku maisha yako yatachukua sura mpya, bora kuliko Jana.

Aina ya pili ni KABURI (Grave/Destroyer/Distraction/Consumer) KABURI ni kitu ambacho kinatumika kuzika, kufukia, kuondoa katika ramani au uso wa nchi, kupoteza kabisa historia ya mtu. Mwanamke aina ya KABURI ni yule ambaye akiingia kwenye maisha ya mtu ni kama upepo unaokuja kuzima mshumaa wa matumaini wa huyu Mwanaume. Kipawa kitazimwa kabisa hatasikika tena, kama alikuwa mwanamichezo ndio anaanza kupoteza mwelekeo, hata hudhuria tena mazoezi, ataanza kugombana na watu wote wa karibu wanaomsaidia mambo ya hapa na pale. Atagombana na manager au promoter wake na yote ni kutokana na influence ya huyu Mwanamke aina ya KABURI. Mwanamke wa hivi hata akiwa na pesa bado uwepo wake kwenye maisha ya Mwanaume hausababishi vitu chanya kutokea. Maana atafanya kila kitu kuhakikisha Mwanaume wake hana amani wala utulivu wa moyo. KABURI linaongozwa na wivu. Lipo tayari kukuharibia hata uwaziri kwa sababu linahisi ukiwa kwenye vikao utapata wanawake wengine. KABURI haliwazi maendeleo, linawaza wivu wa kijinga na starehe.”

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter , Instagram Na Youtube “johnpazia”ili kupata habari Kutoka Kila Kona Ya Mitaa Mbalimbali Duniani Live On Live Masaa 24 Kila Siku.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 22
    Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*