Mjue Eric Lenjima. Mwimbaji Wa Injili Alieanza Kuimba Baada Ya Kushawishiwa Na Msichana Anaempenda.

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 24
    Shares

Anaitwa Erick Lenjima. Anaishi Arusha na ni mhitim wa chuo kikuu cha ushirika moshi 2018.

Yeye ni mtoto wa tatu katika familia yake yenye watoto wanne, wanaume wawili na wanawake wawili kwa sasa baada ya Dada yake mkubwa (first born) kufariki 2002.

Amezaliwa katika familia ya kawaida saana kiuchumi na ameishi na kulelewa katika mazingira ya kawaida saana.

Amesoma shule ya msingi Unga LtD na Secondary Elerai Secondary School zote ziko Arusha. Advance amesoma Kagera shule inaitwa Biharamulo Secondary School.

Alianza kufanya mziki 2004/2005 baada ya kujiunga na kikundi cha Sanaa kilichoitwa YOUNG LIFE alipopelekwa na mama yake baada ya kuona anapoteza muda msingi kwenye mziki kusikiliza na kuimba nyimbo za watu. Alipofika Secondary alikutana na kikundi au club iliyoitwa HEALTH CLUB akajiunga na kuendelea kufanya harakati za mziki lakini kwa kipindi hicho alikua akifanya Bongo flavor nikiwa na Kundi maarufu sana Arusha Jambo Squad na wengineo kama France Jamrack . Hakufanikiwa kutoa nyimbo au kurecord nyimbo yeyote akiwa ndani tya kundi hilo na walikuwa wakifanya acapella.

Alianza kuimba muziki wa injili akiwa Chuo kikuu cha Ushirika MoCu baada ya kukutana na rafiki yake wa kike (Girlfriend) ambae hakupenda yeye kuimba nyimbo za kidunia, Hivyo kubadilisha maneno ya moja ya wimbo wake aliokuwa amemuimbia na kuifanya kuwa Gospel.

Aliingia studio na kufanya Gospel kwa mara ya kwanza June 2017 na kuachia wimbo wake wa kwanza unaoitwa IMPOSSIBLE tarehe 14th July 2017 na kufanikiwa kuingia katika chat za kumi bora za mwenzi wa saba katika tovuti ya GOSPO MEDIA.

Alipata nguvu ya kuendelea na akaachia nyimbo ya pili inayoitwa USINIPITE aliyoifanya akiwa amemshirikisha Stewart na kukamilisha nyimbo mbili kwa mwaka 2017 na nyimbo zote mbili ziliweza kuingia katika nyimbo 100 bora za mwaka 2017 kwa Afrika Mashariki.

Mwaka huu amefanikiwa kuachia nyimbo mbili mpaka sasa hivi moja ikiwa ni UNCONDITIONAL LOVE aliyofanya na Exavery pamoja na Cecilia Mdota pamoja na WASTAHILI aliyofanya na Anco Venna.

Akiongea na johnpazia.com Eric Lenjima Alielezea changamoto anazokutana nazo na kusema; “changamoto ni nyingi ikiwemo kutokuwa na maelewano na migogoro kati yangu na rafiki yangu (girlfriend) sababu nyingi ikiwemo ya kuanza kufahamika na watu wengi hasa wadada. Kupata fedha za kurecord katika studio nzuri na zenye viwango , kubanwa na masomo kwa kipindi chote nilichokuwepo chuoni pamoja na kupoteza marafiki na baadhi ya watu wa karibu ambao mwanzo tulikua tukishirikiana nao mambo ya kidunia”.

Pia Akielezea Mafanikio Alisema; “Mafanikio ni mengi saana nimeyapata katika kumtumikia Mungu, Nimefanikiwa kuitwa katika matamasha mbalimbali na OVERNIGHT nyingi vyuoni kama KCMC , Chuo cha Uhasibu Arusha , MoCu , na MTBC . Pia nilipata nafasi ya kualikwa na kuhudumu katika uzinduzi wa album mpya ya kwaya ya mamajusi na kutimiza kwao miaka 43 ya kwaya hiyo”.

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter , Instagram Na Youtube “johnpazia”ili kupata habari Kutoka Kila Kona Ya Mitaa Mbalimbali Duniani Live On Live Masaa 24 Kila Siku.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 24
    Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*