Jengo Lenye Duka La Nakumatt Labomolewa.

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Shughuli ya ubomoaji wa majengo ambayo imekuwa ikiendelea Kenya kuondoa majumba yaliyojengwa katika maeneo yaliyotengewa barabara na yaliyo kwenye kingo za mito na chemchemi Ijumaa iliathiri jumba lenye moja ya maduka makuu ya Nakumatt, Ukay Mall.

Ubomoaji wa jengo hilo umeanza mapema asubuhi.

Ukay Centre ambayo wakati mwingine hufahamika kama Ukay Mall ni jumba linalopatikana katika mtaa wa Westlands, Kenya na thamani yake inakadiriwa kuwa karibu Kshs1bn.

Ubomoaji wa jumba hilo umetokea siku moja baada ya Mahakama Kuu kukosa kutoa agizo la kuzuia kubomolewa kwake.

Jumba hilo limejengwa karibu na mto Kinagare na zilifurika maji wakati wa mvua kubwa iliyonyesha mwaka 2016.

Ubomoaji wa majengo unafanywa na Mamlaka ya Taifa ya Mazingira Kenya (Nema).

Serikali ya kaunti ya jiji la Nairobi pia imekuwa ikibomoa majengo yaliyojengwa bila idhini.

Alhamisi, Rais Uhuru Kenyatta alisema serikali yake haitalegeza msimamo wake katika kubomoa majengo yaliyojengwa meneo ya chemchemi au katika ardhi ya umma iliyonyakuliwa.

Serikali imesema majengo takriban 4,000 wamepangiwa kubomolewa.

Siku chache zilizopita, serikali ilibomoa jumba lenye mgahawa maarufu wa Java Kileleshwa pamoja na kituo cha mafuta cha Shell kilichokuwa karibu, na baadaye jumba kubwa la kibiahsara la South End Mall karibu na barabara la Langata likabomolewa.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amewatahadharisha wote waliojenga katika maeneo yasiyoruhusiwa kuhamisha mali yao kabla ya ‘bomoa bomoa’ kuwafikia.

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter , Instagram Na Youtube “johnpazia”ili kupata habari Kutoka Kila Kona Ya Mitaa Mbalimbali Duniani Live On Live Masaa 24 Kila Siku.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*