Auawa Kwa Risasi Baada Ya Kuzuka Ugomvi Wa Kudaiana Elfu Thelathini.

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Mlinzi wa kampuni ya Lake Security huko Mwanza, ameuawa kwa kupigwa risasi tumboni na mlinzi mwenzake baada ya kuzuka ugomvi kati yao wa kudaiana Tsh. 30,000.

Kamanda wa Polisi Ahmed Msangi, alimtaja aliyeuawa katika ugomvi huo wa Julai 6 kuwa ni Charles Pendo(24) mkazi wa Bukokwa na aliyefyatua risasi ni Octavian Wilson(35) mkazi wa Mabatini.

Alisema Pendo alipigwa risasa kwa kutumia bunduki aina ya Rifle yenye namba TZCAR 80856 na kufariki dunia papo hapo huku mtuhumiwa wa mauaji hayo alitorokea kusikojulikana.

Mtuhumiwa wa mauaji hayo badi hajakamatwa, huku msako mkali wa kumtafuta katika maeneo mbalimbali ukiendelea.

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter , Instagram Na Youtube “johnpazia”ili kupata habari Kutoka Kila Kona Ya Mitaa Mbalimbali Duniani Live On Live Masaa 24 Kila Siku.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*