Makamu Wa Raisi Ahukumiwa Kutumikia Kifungo Jela.

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 6
    Shares

Makamu wa Rais Mstaafu wa Argentina, Amado Boudou ahukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 5 na miezi 10 jela baada ya Mahakama kumkuta na hatia katika mashtaka ya rushwa.

Bwana Boudou aliyekuwa madarakani kuanzia mwaka 2011 hadi 2015 pamoja na Rais Cristina Fernandez amezuiwa kushika nafasi yoyote ya kiuongozi katika ofisi za umma.

Hukumu hiyo pia imeambatana na kutakiwa kulipa faini ya kiasi cha Shilingi za Kitanzania, Milioni 7,329,367.26

Makamu huyo wa Rais Mstaafu akiwa madarakani alijipatia faida kubwa isivyohalali baada ya kuipa tenda kampuni binafsi ya Ciccone ya kuchapisha fedha za nchi hiyo.

Shauri hili lilianza kusikilizwa mnamo mwaka 2012 ambapo mara kadhaa, bwana Boudou alikana mashtaka haya.

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter , Instagram Na Youtube “johnpazia”ili kupata habari Kutoka Kila Kona Ya Mitaa Mbalimbali Duniani Live On Live Masaa 24 Kila Siku.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 6
    Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*