Ujumbe huu wamkera Manara ‘Kusajili mchezaji kutoka Yanga kwa sasa ni sawa na kula mali ya yatima’

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kuacha kuandika maneno ya dhihaka dhidi ya watani wao wa jadi Yanga na badala yake watumie muda huu kuwasaidia kisaikolojia kutokana na wakati mgumu wa ukata wanao pitia.

Manara ameyaeleza hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram huku akiposti ujumbe unaosomeka ”Kusajili mchezaji kutoka Yanga kwa sasa ni sawa na kula mali ya yatima.”

Nawaonya washabiki wa Simba..ni marufuku kutengenezea vtu kama hvi kwa sasa..tuwasaidie kisaikolojia kurejea ktk hali yao ya kawaida..kuendelea kuwabeza ni kupunguza mapato kwenye makampuni ya simu coz hawatanunua bando la kuingia Instagram na FB

Bila shaka kama wewe ni mpenzi wa mchezo wa soka hapa nchini na mfuatiliaji mzuri utakuwa unafaha hali ya klabu ya Yanga kiuchumi ilivyo mbaya kwa sasa hadi kupelekea waliyokuwa viongozi wao wa kuu kuweka wazi jambo hilo kabla hawajang’atuka ili kuona kama watapata watu wa kuokoa jahazi la timi hiyo kubwa na kongwe nchini.

Licha ya kuwa na mdhamini lakini klabu ya Yanga inapitia kwenyekipindi kibaya zaidi haijawahi kutokea hadi kupelekea viongozi wake wote wakuu kujiuzulu nyazifa zao kwakutoa sababu mbalimbali na timu hiyo kurudishwa kwa baraza la wazamini kwamuda.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*