Ni muda wa Neymar kumfuata Perez apate makombe au kubaki na El Khelaifi ale pesa

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
 • 17
  Shares

Majina 10 ya nyota watakaochuana katika tuzo za mchezaji bora wa Fifa yametoka, lakini habari kubwa ni kutokuwepo kwa mshambuliaji wa Brazil na PSG Neymar katoka orodha hiyo.

Watu wengi wameshangazwa na jambo hilo japo ukiiangalia orodha yenyewe unaweza kubaki kujiuliza Neymar alitakiwa amuondoe nani katika orodha hiyo ili akae yeye?

Raphael Varane ndio aondoke? Hapana huwezi kumuondoa mlinzi kariba ya Varane ambaye mkononi ana kombe la Champions League na ana kombe la dunia na kumuweka mtu ambaye ameshinda tu Ligue 1.

TAKWIMU ZA NEYMAR 2017/2018 PSG

 • MECHI 20
 • DAKIKA 1788
 • MAGOLI 19
 • ASSISTS 13
 • K NJANO 4
 • K NYEKUNDU 1

Pengine dunia imeshtuka sana kuhusu Neymar kutokua katika tuzo hizi lakini tupo wengi pia ambao tuliliona tangu Neymar akikubali pesa za Waqutar £200m na kujiunga na PSG, uhamisho ambao ulionekana wa kifedha zaidi kuliko mafanikio ya mchezaji binafsi.

Pele hakucheza barani Ulaya lakini anatajwa mchezaji bora wa dunia, Diego Maradona achilia mbali alikipiga Barca lakini hata akiwa na Napoli tu dunia ilimtambua kama mchezaji bora wa dunia, muda mwingine sio lazima uwe Barca, Madrid au United ili uwe bora duniani, lakini hiyo ilikuwa zama za wakina Pele. Zama ambazo Perez hakuwepo, Woodward, Abromovich hakuwepo na hakukuwa na nguvu kubwa ya utengenezaji timu kama sasa.

Tumsikilize kwanza Rivaldo “Ufaransa sio kama Ujerumani, sio kama Hispania wala sio kama Uingereza, sio ligi ngumu na haina historia ya Champions League kwa Neymar kuiacha Barcelona na kwenda PSG ni kosa amefanya.”

Baada ya kusikia maneno ya Rivaldo turudi kwenye hoja ya msingi, Neymar amefuata makombe au pesa PSG? hakuna ubishi kwamba ni kweli PSG wanajaribu kutengeneza timu tishio Ulaya lakini 90% uhamisho wa Neymar ulichagizwa zaidi na pesa nyingi alizoahidiwa.

KIASI CHA PESA NEYMAR ANACHOINGIZA PSG.

 • Dakika €70
 • Lisaa €4,200
 • Kwa siku €100,821
 • Wiki €707,692
 • Kwa mwezi €3.07m
 • Kwa mwaka €36.8m

Kwa kiasi hicho cha pesa na wakikumbuka maisha ya dhiki waliyotokea nchini Brazil ni wazi kwamba huwezi tena kuwaza Champions League au kucheza na Neymar na hii ilimfanya Neymar na baba yake kukubali kuacha mpira mzuri na kufuata pesa.

Mchambuzi mmoja nguli wa masuala haya alisikika akisema “kama hutakiwa Real Madrid unaweza kuondoka, lakini kama unaondoka Real Madrid, Barcelona au Bayern Munich na kusema unaondoka kwenda kufuata makombe utakuwa muongo.”

Neymar amejidanganya na ametudanganya kuhusu uhamisho wake PSG kuwa ni wa makombe, na ameanza kuumbuka kwani baada ya hii Fifa Male Player Awards hakuna namna ambayo Neymar anaweza kuwepo katika 3 bora ya Ballon D’or, awepo kwa lipi? Ligue 1? HAPANA.

Amsikilize Kaka na Rivaldo, nyota wa zamani wa Brazil na Real Madrid anampa Neymar ushauri wa kumvusha hapa “huku Brazil ni mtu mkubwa na wengi tunampenda kama mchezaji na Super Star lakini sasa naona ni wakati wa yeye kwenda Real Madrid’

Ndio aende tu Madrid na huu ndio wakati sahihi wa yeye kwenda maana kama Neymar anatafuta ufalme na kucheza nje ya kivuli cha Messi baaasi Real ni mahala pa kutengeneza ufalme katika wakati huu ambapo hakuna mfalme na tena anakwenda kuwa mfalme mwenye makombe na mituzo kibao tofauti na ufalme wa PSG.

Lionel Messi ni kama Neymar tu tena bora Neymar alikwenda hadi robo fainali kombe la dunia wakati Messi aliishia 16 bora lakini Messi yupo kwenye orodha ya wachezaji 10 wa tuzo za Fifa mens player award, hii ni kutokana na ukubwa wa ligi ambayo Messi amechukua kiatu cha ufungaji ni kubwa sana tofauti na alipo Neymar.

Kama ningekuwa mshauri wa Neymar hata leo ningepiga hodi kwa Florentino Perez kumuambia atupe pesa tusaini Real Madrid ndio namna pekee ya Neymar kubeba tuzo, kubaki PSG ni kutaka tu kula pesa za Sheikh Nasser El Khelaifi.

 


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
 • 17
  Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*