“Nusu fainali kombe la dunia 2018 hazina msisimko”-Shaffih Dauda

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 11
    Shares

Kuelekea katika mechi za nusu fainali kombe la dunia Russia, mechi ya kwanza itachezwa leo uwanja wa St Petersburg ambapo Ufaransa watacheza na Ubelgiji, mechi nyingine itakuwa katika jiji la Moscow ambapo England watacheza na Croatia mechi ambayo imekuwa gumzo na imewasafirisha watu wengi kutoka visiwa vya Uingereza kwenda Russia kutoa support kwa timu yao.

Fainali hizi za kombe la dunia ni za tatu kwa Shaffih Dauda kuhudhuria kama mwandishi wa habari. Mara ya kwanza ilikuwa Afrika Kusini mwaka 2010, Brazil mwaka 2014 na sasa Russia.

Kwa upande wake Dauda anasema hatua ya nusu fainali za kombe la dunia mwaka huu hazina msisimko mkubwa ukilinganisha na zile za 2010 na 2014 ambazo alizishuhudia.

“Mwaka 2010 tulishuhudia nusu fainali iliyohusisha timu ya Hispania, Ujerumani, Uruguay na Uholanzi. Uruguay ilikuwa inawakilisha bara la Amerika ya Kusini, Uholanzi, Ujerumani na Hispania zote ziliwakilisha bara la Ulaya.”

“Mwaka 2008 faiali ya EURO ilikuwa kati ya Ujerumani dhidi ya Hispania kwa hiyo ni timu mbiliambazo zilikuwa kwenye peak ya aina yake, miaka miwili baadaye zikafanikiwa kufika nusu fainali ya kombe la dunia Afrika Kusini.”

“Uholanzi ilikuwa na kizazi cha akina Wesley Sneijder na walikuwa na timu nzuri ambayo ilifanya vizuri mwaka huo kwa hiyo timu nne zilikuwa kwenye kiwango kikubwa na ufuatiliwaji ulikuwa mkubwa kutoka kwa wenyeji Afrika Kusini tangu nchi yao ilipotangazwa kuwa mwenyeji.”

“Timu ya wenyeji ilitolewa mapema kwenye hatua ya makundi lakini ilikuwa vigumu kugundua kama mwenyeji hayupo kwenye mashindano kwa namna ambavyo excitement ilivyokuwa imetamalaki maeneo yote.”

“Mwaka 2014 nchini Brazil tulishuhudia nusu fainali iliyohusisha Ujerumani, Brazil (mwenyeji), Argentina pamoja na Uholanzi. Safari hii bara la Amerika liliwakilishwa na timu mbili (Brazil na Argentina) huku Ulaya ikiwakilishwa na top teams kwa wakati huo (Ujerumani na Uholanzi).”

“Kwa hiyo wenyeji Brazil timu yao kufika nusu fainali ukijumlisha na nchi yao kuwa ya soka pamoja na ma-samba kulikuwa na vibe kubwa sana.”

“Hapa Russia) tumeshuhudia kombe la dunia la maajabu, hatuoni mataifa makubwa yaliyotarajiwa kufika nusu fainali. Wenyeji wamejitahidi kufika robo fainali lakini hakuna msisimko mkubwa.”

“Wakati mwingine kitu kinachosababisha msisimko kuwa mkubwa ni idadi ya watu kwenye mataifa husika yanayoshiriki mashindano. Ukiangalia takwimu za mwaka huu (2018) Croatia ina watu zaidi ya 4 million, Ubelgiji 11 million, Ufaransa watu 65 million na England 66 million.”

“Kwa hiyo angalau hizo nchi mbili (England na Ufaransa) zinaweza kupata uwakilishi mwingi wa watu kuja kuzisapoti nchi zao. Brazil watu zaidi ya 200 million kutokuwepo kwake kwenye nusu fainali ni pigo kubwa kwa sababu uwepo wa watu karibia 400,000 waliosafiri kutoka Brazil kuja hapa wanaondoka maana yake wanaacha pengo.”

“Croatia ina watu milioni 4, hawawezi kuja watu zaidi ya milioni 1, Ubelgiji yenye population ya watu 11 million hawawezi kuja watu 2 million kwa hiyo ndiyo maana msisimko ni mdogo nikilinganisha na zile tournament mbili nilizopata kuzishuhudia.”


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 11
    Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*