Mecky Sadick afunguka Tarimba kujiuzulu Yanga

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Abbas Tarimba ameamua kujiondoa kwenye kamati maalum iliyoundwa na Bodi ya Wadhamini ya Yanga kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo katika mambo mbalimbali ikiwemo usajili na kusaidia upatikanaji wa fedha.

Miongoni mwa sababu alizozitoa Tarimba hadi kufikia uamuzi wa kujiuzulu ni kutofurahishwa na namna mambo yanavyokwenda huku akilalamika kamati yao kubezwa.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Said Mecky Sadick amesema bado hana taarifa za kujiuzulu kwa Abbas Tarimba ambaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo.

“Sijawasiliana na mwenyekiti wangu Tarimba, hata kujiuzulu kwake mimi sina taarifa, ningekuwa nimewasiliana nae na akanieleza ningekuwa na lolote la kusema”-Sadick.

“Tangu tulipoteuliwa vimefanyika vikao viwili, kikao cha kwanza sikuhudhuria kikao cha pili tulipokutana tulikubaliana nini kifanyike ili hayo najukumu tuliyopewa tuweze kuyatimiza.”

“Kwa bahati mbaya mimi nipo Mwanza nilitegemea wenzangu ambao karibu wote wapo Dar wangekuwa wanasukuma hayo ambayo tulikubaliana katika kikao cha mwezi uliopita.”

Kwa sasa Yanga inakabiliwa na ukosefu wa fedha tangu alipojiuzulu aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*