Barua ya Adres Iniesta kwa mashabiki zake

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 4
    Shares

Kati ya matokeo ya kustaajabisha katika kombe la dunia 2018 ni baada ya Hispania kuondolewa katika michuano hiyo na timu ya taifa ya Urusi, baada ya matokeo hayo wengi walitabiri unaweza kuwa mwisho wa nyota kadhaa.

Kati ya viungo bora kuwahi kuonekana katika viwanja vya soka ni Andres Iniesta, lakini umri wa Iniesta umekwenda na baada ya matokeo dhidi ya Urusi iliaminika unaweza kuwa mwisho wake kukipiga Hispania, Iniesta ameibuka na barua kwa mashabiki zake na wa Hispania.

“Habarini ndugu zangu?, miaka 14 iliyopita nilivaa jezi ya timu ya taifa ya Hispania kwa mara ya kwanza, nilikuwa na miaka 15 katika kipindi hicho na siwezi kusahau huo wakati.

“Kama ilivyo kwa vijana wengine na kwangu pia ilikuwa ndoto kuvaa rangi za timu yangu ya taifa tayari kwenda kuitetea, hakika kilikuwa kitu cha kipekee sana kwangu na ilikuwa jukumu pia.

“Katika nyakati zote hizi nilizokuwepo nilipambana kwa moyo wote na kutoa kila nilichonacho ili kuweza kuwafanya muvunie uwepo wangu kukosini.

“Najiona mwenye bahati kubwa kuitumikia Hispania hii ambayo ilikuwa na wachezaji bora kabisa, tulifanikiwa katika vitu vingi tulivyotamani lakini pia tulipata makwazo makubwa yasiyokwepeka.

“Nawashukuru wote kwa kunifanya kuwa mchezaji bora na kuwa karibu na wachezaji bora na imekuwa faraja kwangu kuutumikia muda huu wote nikiwa niko na ninyi.

“Lakini baada ya kufikiria kwa zaidi ya mwezi sasa naamini wakati wangu kukaa pembeni umefika, sina mashaka na wachezaji wajao na daima nitabaki kama shabiki mkubwa wa timu ya taifa ya Hispania”

Iniesta alikuwepo katika timu ya taifa Hispania iliyobeba kombe la dunia mwaka 2010, lakini vile vile alikuwepo wakati wakishinda Euro mwaka 2008 wakaja tena wakashinda taji hilo la Euro mwaka 2010.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 4
    Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*