Utafiti: Matumizi mabaya ya vitambaa vya jikoni ni hatari kwa afya

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
 • 4
  Shares

Matumizi mbalimbali ya vitaulo vya jikoni huweza kusababisha vijidudu vya sumu kwenye chakula, utafiti umeeleza.

Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Mauritius walichunguza vitambaa 100 vya jikoni vilivyokuwa vikitumika kwa kipindi cha mwezi mmoja

Waligundua kuwa bakteria aina ya E.coli anaweza kupatikana kwenye vitambaa ambavyo vimetumiwa kwa kazi zaidi ya moja jikoni, kama vile, kufutia vyombo na kufutia meza pia kukaushia mikono.

Matumizi hayo yanaongeza hatari ya kusambaa kwa bakteria wanaoweza kusababisha usumu kwenye chakula.

Serikali ya Mauritius imesema kuwa vitambaa vya jikoni, sponji na vitambaa maalum vya kushikia vitu vya moto vinapaswa kuoshwa au kubadilishwa mara kwa mara, pia vinapaswa kuoshwa na kuanikwa vikauke kabla ya kutumika tena.

Utafiti huu umewasilishwa katika mkutano wa mwaka wa Baiolojia nchini Marekani.

Miongoni mwa vitaulo vilivyokusanywa, asilimia 49 vilikuwa na bakteria, ambao waliongezeka kwa idadi yao kutokana na ukubwa wa familia inayotumia vitambaa hivyo, uwepo wa watoto na ongezeko la familia.

E.coli ni aina ya bakteria ambaye hupatikana kwenye utumbo wa binaadamu na mnyama.Mara nyingi hawana madhara lakini wanaweza kusababisha sumu kwenye chakula na maambukizi.

Ni kwa namna gani utaweza kuzuia vijidudu kusambaa jikoni?

 • Badilisha vitambaa vya kufutia vyombo mara kwa mara.
 • Baadhi ya wataalam wanasema badilisha kila siku ambazo utakuwa unapika.
 • Tumia vitambaa ambavyo baada ya matumizi yake hutupwa au vitambaa mithili ya karatasi.Hivi vitakomesha kusambaa kwa vijidudu.
 • Vitambaa ambavyo vitaendelea kutumiwa vinapaswa kufuliwa kila baada ya matumizi .
 • Hakikisha mahali utakapoweka chakula ni pasafi kabla ya kuanza kutumia.
 • Tumia mbao tofauti za kukatia kwa vyakula tofauti ambavyo havijapikwa kama vile nyama mbichi na vyakula vingine ambavyo havihitaji kupikwa.
 • Safisha sehemu uliyopikia baada ya mapishi.

”Data zimeonyesha kuwa mapishi yanayofanyika katika mazingira yasiyo safi hufanyika kwenye makazi ya watu wengi”, ameeleza Kiongozi wa utafiti huo, Dokta Susheela Biranjia-Hurdoyal.

”Taulo mbichi na matumizi yake kwa kazi mbalimbali vinapaswa kuepukwa.Familia kubwa zenye watoto na wazee zinapaswa kuzingatia usafi wa jikoni.Alieleza Dokta.

Source;bbc swahili

iunge nasi kupitia Facebook, Twitter , Instagram Na Youtube “johnpazia”ili kupata habari Kutoka Kila Kona Ya Mitaa Mbalimbali Duniani Live On Live Masaa 24 Kila Siku.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
 • 4
  Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*