Mtoto Afariki Akiombewa Na Mchungaji.

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 22
    Shares

Mtoto ambaye alikuwa ni mgonjwa amefariki baada ya wazazi wake kumpeleka kuombewa na Mchungaji wa kanisa la ‘Kanitha Ya Ngai’ ambaye haruhusu waumini wake kutumia tiba za kisasa.

Wazazi hao kwa sasa wamekamatwa na Polisi katika kijiji cha Kinungi kaunti ya Nakuru nchini Kenya huku Mchungaji huyo akitokomea kusikojulikana.

Katika eneo la Kinungi kunatajwa kuwa na waumini wengi wa kanisa hilo ambao hawaamini katika tiba za kisasa.

Mzazi wa kwanza kukamatwa alikuwa ni mzazi wa kike ambaye alikamatwa baada ya kwenda kuomba kibali cha kumzika mtoto wake kwa Chifu wa eneo hilo.

Kwa mujibu wa Chifu, visa vingi vya waumini hao vimeongezeka sana kwa siku za hivi karibuni na amesema kuwa kwa sasa wanamtafuta mchungaji huyo ambaye amekimbia baada ya kusikia anatafutwa ili ahojiwe.

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter , Instagram Na Youtube “johnpazia”ili kupata habari Kutoka Kila Kona Ya Mitaa Mbalimbali Duniani Live On Live Masaa 24 Kila Siku.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 22
    Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*