Tanzia; Mama Wa Rc Gambo Afariki Dunia.

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amefiwa na mama yake mzazi usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya The Madras Medical Mission – Chennai nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Rc Gambo Ameandika Katika Mitandao Ya Kijamii “Kwa masikitiko na uchungu mkubwa napenda kutangaza kifo Cha Mama yangu Mzazi ( Mama aliyenilea kwa kuuza uji) kilichotokea usiku wa leo kwenye hospitali ya The Madras Medical Mission – Chennai nchini India! Kama mtoto nilijitahidi kufanya kila lililowezekana ikiwa ni pamoja na kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu kabla ya India. Ni Imani yangu kuwa hata Mungu atakubali kuwa kama binadamu nilifanya kila lililowezekana Ila yeye kampenda zaidi! Niombeeni sana maana mtihani huu ni mzito sana kwangu sidhani kama nita uhimili!

Tutawajulisha taratibu za mazishi Muda si mrefu!

Hizi Ni Baadhi Ya Picha Za Mama Huyo Akiwa Hospitali:

Jiunge nami kupitia Facebook, Twitter , Instagram Na Youtube “johnpazia”ili kupata habari Kutoka Kila Kona Ya Mitaa Mbalimbali Duniani Live On Live Masaa 24 Kila Siku.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*