Goodluck Gozbert Asema Haya Siku Ya Birthday Yake.

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 21
    Shares

Jana Tarehe 12 April Ni Siku Ya Kumbukizi Ya Kuzaliwa Muimbaji Maarufu Wa Gospel Hapa Nyumbani Tanzania Goodluck Gozbert.Ikiwa Zimepita Siku Mbili  toka ufanyika uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam, Ambapo Mwimbaji Wa Nyimbo Za Injili Goodluck Gozbert Alipata Nafasi Ya Kuhudumu Katika Uzinduzi Huo Wimbo Mpya ‘Hawawezi Kushindana’ Mbele Ya Raisi Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.

 

Jana Siku yake Ya Kuzaliwa Kupitia Ukurasa Wake Goodluck Gozbert Ameandika

Nikukumbushe Tu….Sikuzaliwa Kwenye Familia Yenye Kujulikana au Kuwa Na Heshima Kokote Kule, na Wala Sikuwahi Kushika hata Nafasi Ya Tano Darasani, Nakumbuka Kuchekwa, Kukatishwa Tamaa, Kuandikiwa Ubaya, Kunenewa Uongo Na Kutabiriwa Kushindwa kila Nilipofikiri Ningeweza, Nakumbuka Mengi Mengine Ya Juzi Tu…..!!!! Ila Hakuna kitu nakumbuka Zaidi Kama Zile Ahadi Za Mungu Kwangu, Hakuna Kitu Nakumbuka Kama Huruma Za Huyu Yesu Aliyenipenda Nikiwa Sijielewi…..!!!! Kesho Nitawaambia Wanangu, Mungu Aliyenitoa na Kunifikisha Pale Ndiye Atakayeenda Pamoja Nanyi.”

Jiunge nami kupitia Facebook, Twitter , Instagram Na Youtube johnpazia”ili kupata habari Kutoka Kila Kona Ya Mitaa Mbalimbali Duniani Live On Live Masaa 24 Kila Siku.

 


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako
  • 21
    Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*