OZIL ATUPIA UJERUMANI IKIIFUMUA NORWAY 6-0, LAKINI BADO KOMBE LA DUNIA

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

 

Ujerumani imeshinda kwa mabao 6-0 dhidi ua Norway lakini bado haijajihakikishia kufuzu Kombe la Dunia. Mesut Ozil alifunga bao moja huku akiwa kiungo muhimu kwa kuwa alikuwa katika kiwango bora.
Ushindi wa Ireland Kaskazini wa mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech unaifanya Ujerumani isiwe na uhakika wa asilimia mia.
Wengine waliofunga mabao katika mechi hiyo ya Kundi C baada ya Ozil kufunga la kwanza ni Julian Draxler, Timo Werner aliyefunga mawili, Leon Goretzka na mkongwe Mario Gomez aliyepigilia msumari wa mwisho.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*