Sharapova atupwa nje ya michuano ya US Open

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Mcheza tenisi raia wa Urusi, Maria Sharapova ameyaaga mashindano ya wazi ya Marekani (US Open) baada kukubali kipigo kutoka kwa mwanadada, Anastasija Sevastova katika mzungungo wa nne.

Ikiwa ni michuano yake ya kwanza ya Grand Slam toka akae nje ya uwanja kwa mwaka mmoja na miezi 7 amekubali kipigo cha jumla ya seti 5-7 6-4 6-2 kutoka kwa Sevastova aliyetinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo huko New York.

Sevastova mwenye umri wa miaka 27 sasa anatarajia kukutana na mmarekani, Sloane Stephens katika hatua ya robo fainali baada ya kumfunga Julia Goerges.

Sharapova mwenye umri wa miaka 30 amesema

“Ulikuwa mchezo mzuri sana wa wiki iliyopita, nimejifunza mengi na ilikuwa nafasi muhimu kwangu na shukuru sana kwa kupata nafasi hiyo”, amesema Maria Sharapova.

By Hamza Fumo


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*