Wayne Rooney aingia matatani na polisi

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Baada ya kuachana na timu ya taifa huku msimu huu akiwa katika kiwango kizuri sana na Everton lakini usiku wa jana mshambuliaji Wayne Rooney alijikuta matatizoni na polisi nchini Uingereza.

Wayne Rooney alikamatwa usiku wa jana na mapolisi katika eneo jirani kabisa na kwake kwa kile kinachodaiwa kwamba alikuwa akiendesha gari lake huku akiwa amelewa pombe.

Rooney alikamatwa karibia na uwanja wa mazoezi wa Finch Farm ambao unatumiwa na klabu ya Everton kwa ajili ya mazoezi ambapo pia ndio jirani na eneo ambalo amekuwa akiishi kwa muda wa miaka 12 sasa.

Inasemekana jana jioni mshambuliaji huyo aliamua kutoka out lakini wakati akiwa anarejea nyumbani polisi walihisi atakuwa amelewa pombe na ndipo waliamua kumfuata kwa nyuma na kumsimamisha.

Rooney amekuwa akiandamwa sana na kesi zinazohusiana na masuala ya ulevi na kama unakumbuka mwaka jana akiwa United alipigwa picha akionekana chakari baada ya mchezo wa England dhidi ya Scotland.

Pia habari za Wayne Rooney kuendelea kupiga pombe zimefika siku chache baada ya mkewe Coleen kuionesha dunia kwamba wanatarajia mtoto wa nne na mwanasoka huyo aliyestaafu kuichezea Uingereza.


Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*