Ndoto ya Usain Bolt kucheza Manchester United huenda ikatimia Mwezi Septemba mwaka huu

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

 

Huenda ndoto ya Mwanariadha kutoka Jamaika Usain Bolt kucheza Mpira wa Miguu katika Dimba la Old Traford ikatimia Septemba 2 wakati Timu ya Wachezaji wakongwe wa  Manchester United itakapokutana na Maveterani wa Klabu ya Barcelona.

Bolt ambaye ni Mshindi mara nane wa Medali ya Dhahabu katika Mashindano ya Olimpiki amejumuishwa kwenye kikosi cha Manchester United licha kusumbuliwa na jeraha la Msuli wa paja ambalo amepata katika Mashindano ya Dunia ya Championship yaliyofanyika London yakiwa ndio Mashindano yake ya Mwisho baada ya kutangaza kustaafu.

Mwanariadha huyo anayesadikika kuwa ni Binadamu mwenye kasi zaidi Duniani ni Shabiki wa Manchester United na amekuwa na hamu ya kucheza ndani ya kikosi cha United kwa muda mrefu sana, Mwaka 2012 alitembelea Old Traford na kupewa Jezi ambayo iliandikwa ‘Bolt 9.63’ ambayo ilikua na maana ya Muda ambao Mwanariadha huyo alitumia katika Ushindi wa Medali ya Dhahabu katika Mashindano ya Olimpiki 2012.

Katika Mchezo huo wa United dhidi ya Barcelona utakaopigwa Septemba 2 Kikosi cha United kitaongozwa na Bryan Robson ambaye ni Nahodha wa Zaamani wa kikosi cha hicho huku kikiundwa na Wachezaji wengine ambao ni Andy Cole, Edwin van der Sar, Paul Scholes, Jesper Blomqvist, Denis Irwin, Ronny Johnsen, Dwight Yorke, Wes Brown, Phil Neville, Louis Saha, Mikael Silvestre, Quinton Fortune, Dion Dublin pamoja na Usain Bolt.

Kwa upande wa Barcelona kikosi kitaongozwa na Kocha Mari Bakero huku kikiundwa na Wachezaji wengine wakiwemo Gaizka Mendieta, Eric Abidal, Migel Angel Nadal pamoja na Gheorghe Popescu.

Sambaza Upendo , Share na Rafiki zako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*